Luke 9

Isa Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

1 aIsa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2 bkisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3 cAkawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 4 dKatika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 5 eKama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 6 fHivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Herode Afadhaika

(Mathayo 14:1-12; Marko 6:14-29)

7 gBasi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yahya Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu. 8 hWengine wakasema Ilya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. 9 iHerode akasema, “Yahya nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ambaye ninasikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona.

Isa Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14)

10 jMitume wake waliporudi, wakamweleza Isa yote waliyofanya. Akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji uitwao Bethsaida. 11 kLakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.

12 lIlipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

13Isa akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.”
14Walikuwako wanaume wapatao 5,000.

Isa akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.”
15Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. 16 mIsa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. 17Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

Petro Amkiri Isa Kuwa Ndiye Al-Masihi

(Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29)

18 nWakati mmoja, Isa alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

19 oWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya Mbatizaji, wengine husema ni Ilya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

20 pKisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
wa Mungu.”

21 rIsa akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo. 22 sIsa akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”

23 tKisha akawaambia wote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate. 24 uKwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. 25 vJe, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au kuangamiza nafsi yake? 26 wMtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba, pamoja na malaika watakatifu. 27 xAmin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu.”

Bwana Isa Abadilika Sura

(Mathayo 17:1-8; Marko 9:2-8)

28 yYapata siku nane baada ya Isa kusema hayo, aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana, akaenda nao mlimani kuomba. 29Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi. 30Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Musa na Ilya, wakizungumza naye. 31 zWalionekana katika utukufu wakizungumza na Isa kuhusu kifo chake ambacho kingetokea huko Yerusalemu. 32 aaPetro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 abMusa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, “Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” Lakini Petro alikuwa hajui asemacho.

34Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu, likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu. 35 acSauti ikatoka kwenye lile wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, niliyemchagua. Msikieni yeye.” 36 adBaada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Isa akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona.

Kuponywa Kwa Kijana Mwenye Pepo Mchafu

(Mathayo 17:1-8; Marko 9:2-8)

37 ae afKesho yake waliposhuka kutoka mlimani, alikutana na umati mkubwa wa watu. 38Mtu mmoja katika ule umati wa watu akapaza sauti, akasema, “Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee. 39Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache. 40Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.”

41 agIsa akawajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”

42 ahHata yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo mchafu akamwangusha, akamtia kifafa. Lakini Isa akamkemea yule pepo mchafu amtoke, akamponya yule mtoto, na akamrudisha kwa baba yake. 43Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu.

Wakati bado watu walikuwa wanastaajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Isa, yeye akawaambia wanafunzi wake:
44 ai“Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.” 45 ajLakini wao hawakuelewa alimaanisha nini. Maana ya maneno hayo ilifichika kwao, hivyo hawakuyaelewa, nao wakaogopa kumuuliza maana yake.

Ni Nani Atakayekuwa Mkubwa Kuliko Wote

(Mathayo 18:1-5; Marko 9:33-37)

46 akKukazuka mabishano miongoni mwa wanafunzi kuhusu ni nani miongoni mwao atakayekuwa mkuu kuliko wote. 47 alLakini Isa akayatambua mawazo yao, naye akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kando yake. 48 amKisha akawaambia, “Yeyote amkaribishaye mtoto huyu mdogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi, na yeyote atakayenikaribisha mimi, atakuwa amemkaribisha yeye aliyenituma. Kwa maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu, ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

49 anYohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”

50 aoIsa akasema, “Msimzuie, kwa sababu yeyote ambaye si kinyume nanyi, yu upande wenu.”

Isa Akataliwa Samaria

51 apWakati ulipokaribia wa yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu. 52 aqAkatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu; 53 arlakini watu wa kijiji kile hawakumkaribisha kwa sababu alikuwa anakwenda zake Yerusalemu. 54 asWanafunzi wake, yaani Yakobo na Yohana, walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuagize moto kutoka mbinguni ili uwaangamize?” 55Isa akageuka na kuwakemea, 56 atnao wakaenda kijiji kingine.

Gharama Ya Kumfuata Isa

(Mathayo 8:19-22)

57 auWalipokuwa njiani wakienda, mtu mmoja akamwambia Isa, “Nitakufuata kokote uendako.”

58 avIsa akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

59 awIsa akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.”

Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

60 axIsa akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.”

61 ayMtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa yangu.”

62Isa akamwambia, “Mtu yeyote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
Copyright information for SwhKC